Sunday, April 26, 2020

Jifunze kuitambua Aina yako ya Ngozi

VIPI UNAWEZA KUJUA AINA YA NGOZI YAKO?

Pale ambapo unajitahid kufanya kila kitu kwa ajili ya Ngozi yako kupendeza na kuwa yenye afya, halafu ukahisi Kama inakusaliti hivi najua huwa utakua na wasiwasi na kutokujisika huru muda wote. Pengine utakua unascrub uso wako kwa kila wiki, moisturizing na vengine kila baada ya muda fulani lakini hakuna matokeo yoyote unayoyapata zaidi ya kuongeza tatizo. Basi inakupasa kuelewa kwamba, Kupata matokeo mazuri katika utunzaji wa ngozi ni lazima uzingatie yafuatayo:
1.kuijua aina ya ngozi yako.
2. Kupata ushauri vizuri kuhusiana na bidhaa ambazo unatumia.
3.kutumia products sahihi na salama kulingana na mahitaji ya ngozi yako.

Nakala hii itakusaidia wewe kuelewa ni ipi  Aina ya Ngozi yako ili uweze kuwa mchaguzi sahihi wa products zako kulingana na Ngozi yako. Twende pamoja👇

#kitu cha kwanza unachotakiwa kufanya hakikisha kwamba ngozi yako ya uso haina make up wala moisturizer wala toner wala kipodozi cha aina yoyote. Baada ya hapo nawa uso wako kwa sabuni ya kawaida halafu acha Ngozi yako ikauke kwa masaa 2-3. katika kipindi Hichi hakikisha hupaki kitu chochote Kama vile lotion, wala kugusa gusa uso wako.  Anza kuichunguza kwa makini Ngozi ya uso wako. 

Chukua kioo na uanze kuiangalia kwa umakini Sana huku ukifuatilia chochote kile kitakachojitokeza.  Hapa nimeweka aina za ngozi pamoja na alama zake za kukujulisha kama una ngozi ya aina hiyo

1. Ngozi ya kawaida
Hii itakua ipo Laini, haina mikunjo, wala haipo kavu Sana wala haipo na mafuta mengi.
2. Ngozi ya mafuta.
Chukua tishu yako na ueke kwenye uso wako kwa muda kidogo, kisha itoe na uichunguze tishu yako, ikiwa itakua na mafuta sehemu yote uliyoweka katika uso, basi wewe utakua katika kundi hili.
3. Ngozi kavu.
Ikiwa Ngozi yako utaiona imekaza, na imeanza kujikunja kunja, na wala haina mafuta basi ujue wewe upo hapa.
4.Ngozi mchanganyiko.
Hii ni ya aina ya Ngozi ina mchanganyiko wa mafuta na ukavu. Ngozi ya mafuta itakua katika T-zone na sehemu iliyobakia ni kavu.

Zingatio: Utakapoifahamu vizuri Ngozi yako itakurahisishia wewe kutumia products sahihi, kwa mfano Ngozi yako ni  kavu utatumia products zenye kuleta mafuta kidogo katika Ngozi yako.. Vile vile kwa wenye aina nyingine za ngozi pia huwa rahisi kuelewa ni zipi products sahihi  na njia sahihi za wao kutunza ngozi zao.  Fanya zoezi hili na utumbie ngozi yako ni ya aina gani?

©mwanaaurembo

No comments:

Post a Comment