IFAHAMU AINA YA NGOZI YAKO.
Kitu cha kwanza ambacho ni muhimu katika utunzaji mzima wa afya ya ngozi ni lazima uifahamu aina ya ngozi yako. kuifahamu Ngozi yako itakupelekea urahisi wa wewe kukuambia ni vitu gani unatakiwa kutumia kwa ajili ya kupendezesha Ngozi yako na kuwa yenye afya, na vitu gani hutakiwi kutumia kwa ajili ya kuilinda Ngozi yako.
Hivo basi ningependa kuwachambulia Aina za Ngozi ili uweze kujitathmini mwenyewe upo katika kundi gani?? kwa kawaida Ngozi imegawika sehemu kuu nne na nitaelezea aina moja moja Kama ifuatavyo:

1. Ngozi ya kawaida (Normal skin). Hii ni Aina ya Ngozi ambayo sio kavu sana na wala haina mafuta mengi na Ngozi hii ni nzuri na yenye kupendeza mda wote na pia ni ngozi yenye afya. Ikiwa una Ngozi ya Aina hii huhitaji matunzo makubwa ila usiache kuifanyia matunzo Ngozi yako na kuepuka vile ambavyo vitaharibu Ngozi yako. Kwa kawaida ngozi hii inapatika sana kwa watoto wachanga kwani bado ngozi zao hazijakua affected na chemicals kali ambazo zinapatika katika products kama lotion, cream na zenginezo.
2. Ngozi kavu(dry skin). hii ni Aina ya Ngozi ambayo haina mafuta stahili na haiko na unyevu stahili, kwa kawaida pia ngozi hii huwa imekakamaa kutokana na ukosevu wa unyevu na kiwango kidogo cha mafuta. hivyo basi Ngozi ya Aina hii ni Mara moja kufanya mikunjo (wrinkles). My dear friend unaweza kuwa na miaka 22 ila Ngozi yako iko na miaka 25. I mean ngozi yako ni rahisi kuzeeka na kupata michubuko.
3.Ngozi yenye Mafuta mengi (oily skin). Hii ni Aina ya Ngozi ambayo inangara sana kutokana na wingi wa mafuta na ni Mara moja kunaswa na vumbi na kuchafuka Kwasababu tuu iko na mgandomgando. Pia watu ambao wana aina hii ya ngozi huwa na tundu kubwa usoni ambazo huonekana kwa ukaribu. Sio hivo tuu ila pia Ngozi ya Aina hii ni Mara nyingi husumbuliwa na matatizo ya chunusi.
4. Ngozi mchanganyiko (combination skin). Hii ni Aina ya Ngozi ambayo ni ngumu Sana na yenye shida Sana Kuitambua unaweza kuwa na ngozi ya mchanganyiko lakin ukawa unasema una ngozi ya mafuta kwasabb tu kuna tabia zinafanana. Ngozi hii inakua ina mchanganyiko wa mafuta na ukavu. Sehemu za mafuta ni (T- zone) kutokea kikomoni, puani na kidevuni. Na sehemu iliyobakia ya mashavuni ni sehemu kavu.
Usiwe na waswas juu ya Ngozi ya uso wako.. Ukiifahamu vizuri unaweza kuwa ni mtunzaji mzuri WA Ngozi. Ifahamu Ngozi yako ili uelewe ni nini kifanyike katika kutunza Ngozi yako.
Usiwe na waswas juu ya Ngozi ya uso wako.. Ukiifahamu vizuri unaweza kuwa ni mtunzaji mzuri WA Ngozi. Ifahamu Ngozi yako ili uelewe ni nini kifanyike katika kutunza Ngozi yako.
©mwanaaurembo
No comments:
Post a Comment